Description
Endapo maisha ni safari basi Sokoro amesafiri. Mawimbi yamemzonga na kumsukuma kila upande upande. Macho halisia akayafumba lakini Jicho la Tatu hakulifumba katu. Amelala katika safari hii maana mtu lazima apumzike, akafumba macho halisia lakini Jicho la Tatu hakulifumba katu! Chemichemi na punje za uchafu zikamwingia katika macho halisia akayafikicha lakini Jicho la Tatu hakulifikicha.
Jicho la Tatu halifumbwi halifikichiki maana haliingiwi na uchafu na halilali. Je, hili ni jicho lipi? Je, katika kujenga kichuguu Mchwa ana jicho hilo? Talii hadithi hii ya Jicho la Tatu ili kujipatia majibu.
Vitabu vingine vya hadithi vinavyochapishwa na KLB kwa kiwango hiki ni:
- Ngoma za Uchawi
- Kusema Ukweli
- Ndoto ya Riziki
- Ndoto za Matumaini
- Masaibu Mbugani
- Taabu Taabani
- Titi la Mama I
Reviews
There are no reviews yet.