Description
“Wapo wale wanaokoga kwa mafuta kweli. Hata dunia ikijaribu kuwakwangura kwa kucha zake kubwa, ngumu na katili, haiwawezi. Sisi tulioundwa kwa chuma, tujifanyao wenye nguvu wa kufanya kila aina ya kazi ndio tunaokwaruzwa kwa kucha katili za dunia. Kwani hii dunia tuliitendea nini? Wanasiasa ndio wale wale, waongo! Ooo!
Nitawaletea mabomba ya maziwa, nitainunulia kila kata trekta ya kulimia, kila mkulima atapewa pembejeo bure, vijana watalipiwa karo na waliomaliza masomo kuajiriwa. Miaka mitano baadaye hadithi ni ile ile tu na kama waliopagawa tunawapigia kura. Mnapewa vya bwerere huku ushuru ukiongezeka. Wanakupa mnofu kwa mkono wa kushoto na kukunyang’anya ng’ombe mzima kwa mkono wa kulia…” Tambua hali ya maisha ya Tumaini kwa kusawiri hadithi hii.
Vitabu vingine vya hadithi vinavyochapishwa na KLB kwa kiwango hiki ni:
- Chozi Langu
- Maisha na Vigeugeu
- Hatosheki
Reviews
There are no reviews yet.